Maswali yanayo ulizwa mara kwa mara

Maswali ya Mara kwa Mara

Una swali kuhusu bidhaa au huduma yoyote ya Tunzaa? Maswali yaulizwayo mara kwa mara yamepangiliwa kulingana na mada, na yanatoa majibu ya maswali mengi watumiaji wetu wanauliza. Kama hujapata jawabu unalolitaka, tafadhali tutumie barua pepe kupitia mambo@tunzaa.co.tz

AKAUNTI NA MALIPO

Tunzaa ni nini?

Tunzaa ni jukwaa linalokuza tabia chanya za matumizi ya kifedha kwa vijana wa Kiafrika kupitia teknolojia ya simu za mkononi ikiwa na soko kwa ajili ya bidhaa na huduma.

Kupitia soko letu la bidhaa na huduma tunaunganisha biashara na mtandao wa wanunuzi na kusaidia wanunuzi kufikia malengo na mipango yao kwa kuwezesha malipo ya bidhaa na huduma kwa kiwango kidogo cha pesa kwa kasi ya mtumiaji mwenyewe moja kwa moja kutoka kwenye simu zao.

Je! Ninahitaji akaunti kununua kutoka Tunzaa?

Ndio, unatakiwa kujiunga ili kufanya malipo ya bidhaa au huduma na Tunzaa.

Ikiwa nitaweka namba yangu ya simu kuna malipo yoyote?

Hakuna malipo wakati unajisajili na namba yako ya simu. Namba yako ya simu hutumiwa tu kwa madhumuni ya kukutumia ujumbe wa kukumbusha malengo yako. Pia hutumika kama jina la mtumiaji na inakuwezesha kuingia katika akaunti yako.

Kuna riba ninapofanya malipo na Tunzaa?

Hakuna riba yoyote unapotumia Tunzaa kufanya malipo ya bidhaa au huduma.

Je! Ninaweza kufanya malipo na namba yangu tu?

Hapana, sio lazima. Unaweza kupata msaada kutoka kwa familia, jamaa au rafiki kutimiza malengo yako.

Je! nikianza kulipia bidhaa halafu ikashuka bei sokoni wakati bado nailipia inakuwaje?

Kwa kuwa tayari utakuwa umeshaanza kulipia bidhaa yako, utaendelea kulipia kwa bei ile ile.

BIDHAA

Tunzaa inadhibitije ubora wa bidhaa/huduma kutoka kwa wafanyabiashara?

Tunzaa inahakikisha ubora wa huduma kwa wateja kwa kukagua watoa huduma wetu na pia tunazingatia bidhaa halisi na huduma zenye ubora wa juu.

Naweza kuona bidhaa ambazo watu wengi wanazinunua zaidi?

Kwa sasa tunafanyia kazi huduma hii, tukimaliza majaribio kila mtumiaji wa jukwaa letu ataweza kuona bidhaa zinazonunuliwa zaidi.

Nikinunua bidhaa naipatajee? 

Baada ya kukamilisha malipo, utapokea ujumbe kuhusu malipo yako. Unaweza kuchagua kuifata bidhaa yako au kuletea eneo ulilopo..

Gharama za kuletewa bidhaa ni zipi?

Tunzaa tunatoa huduma ya kukuletea bidhaa yako bure kwa Dar es salaam.

Nitajuaje kama bidhaa yangu bado ipo wakati naendelea kuilipia?

Tunzaa tunahakikisha bidhaa unayoilipia inakuwepo kwa mfanyabiashara hadi pale utakapokamilisha malipo yako.

Ikiwa muda niliojiwekea kukamilisha lengo umefika na sijamali kulipia inakuwaje?

Tunzaa inakuwezesha kufatilia malipo yako wakati wote pia kupokea ukumbusho kuhusu mahitaji yako, hivyo ni rahisi kukamilisha malengo yako.

BIASHARA

Je, ninawezaje kujiunga kama biashara?

Ni rahisi sana. Kwanza pakua aplikesheni ya Tunzaa+ (Aplikesheni  ya biashara) na kisha andikisha biashara yako. Utapokea ujumbe wa kuthibitisha biashara yako.

Je! Ni gharama gani kujiunga kama biashara kwenye Tunzaa?

Kujiunga na kuanza kuuza kwenye Tunzaa ni bure. Aplikesheni ya biashara inakuwezesha kuweka bidhaa au huduma zako kwenye soko la Tunzaa, kufuatilia mauzo yako, kutoa huduma kwa wateja na kukuza biashara yako kwa urahisi.

Biashara yangu ni ya mtandoni na haina leseni ya TRA. Je, bado naweza kujiunga na Tunzaa kama mfanyabiashara?

Tunzaa tunazingatia ubora wa huduma tunayotoa kwa wateja na tunafata sheria zilizowekwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ikiwa unataka kuandikisha biashara yako kwenye Tunzaa hakikisha biashara yako imesajiliwa.

Inawezekana kudhibiti kikomo cha muda wa mnunuzi kumaliza malipo yote ya bidhaa au huduma?

Ndio mfanyabiashara anaweza kupanga muda maalum ambao anapenda mteja awe amekamilisha malipo ya lengo lake.

Mfanyabiashara anatakiwa kulipa kiasi gani kwa Tunzaa ili kuweka bidhaa au huduma zake?

Hakuna malipo. Kujiandikisha Tunzaa na kuanza kuuza bidhaa au huduma ni bure. Utalipia ada ndogo tu pale utakapomilisha mauzo na Tunzaa.

Tunzaa inafaidika vipi na huduma zake?

Tunatoza ada ndogo kwa mfanyabiashara aliyeuza kupitia Tunzaa ili kufidia gharama za mchakato wa malipo na uendeshaji.

Mteja akianza kulipia bidhaa au huduma fedha zinakwenda wapi?

Mteja akianza kufanya malipo ya bidhaa au huduma, fedha anayolipa inatumwa kwenye akaunti ya mfanyabiashara husika.