Tunzaa inatoa siku 7 kurudisha bidhaa ambazo zinakidhi vigezo vya kurudishwa. Tafadhali wasiliana nasi kupitia njia yoyote ya mawasiliano ndani ya siku 7 tangu upokei bidhaa husika na tutahakikisha unapata suluhisho.
HATUA YA 1: Tuma Ripoti
Pia jumuisha picha za bidhaa (pamoja na maelezo kama vile "serial namba", aina, na mengineyo) tuma kwenda mambo@tunzaa.co.tz kama sehemu ya ushahidi.
HATUA YA 2: Kurudisha baada ya Uidhinishaji
Mara tu ombi lako litakapothibitishwa, tutakupa taarifa juu ya njia zinazofaa zaidi za kupata bidhaa kutoka kwako.
HATUA YA 3: Pata Suluhisho
Baada ya uthibitisho wetu wa kupokea risiti ya bidhaa husika, Tunzaa itahusika kukusaidia kumjulisha Muuzaji kufanyia kazi maombi yako na haitahusika na majukumu mengine.
MUHIMU: Weka bidhaa husika kwenye kifurushi chake halisi, ikiwa ni pamoja na vifaa, vitambulisho, lebo au zawadi za bure. Ikiwa umeweka nenosiri kwenye kifaa unachotaka kurudisha, tafadhali hakikisha imeondolewa, vinginevyo, kurudisha kwako kutakuwa batili.
Bidhaa ambazo hazistahili Kurudishwa
- Bidhaa ambazo zimebadilishwa kutoka kwenye kifungashio chake cha asili au kufunguliwa na mtu asiye na idhini ya kufanya hivyo.
- Bidhaa zinazoharibika haziwezi kurudishwa isipokuwa kwa sababu maalum utakazozitoa wakati wa kupokea bidhaa.
- Bidhaa zilizoharibiwa kwa sababu ya matumizi mabaya.
- Vitabu na CD.
- Matengenezo yasiyoruhusiwa, matumizi mabaya, uzembe, unyanyasaji, kuloweshwa na maji, ajali, mabadiliko, matatizo ya ubora wa bidhaa yaliyosababishwa na usakinishaji usiofaa, au lebo zilizobadilishwa namba ya mashine au alama ya bandia;
KURUDISHIWA PESA
Mara tu tutakapopokea bidhaa iliyorudishwa kutoka kwako, tutakagua na kushughulikia kurudisha pesa yako kati ya siku 10 za kazi kwenye namba ya simu uliyotumia kujisajili kwenye Tunzaa.
Tunzaa inatoza 25% ya pesa ambazo tayari umelipa kwa kila urejesho. Tunatoza 25% kulipia gharama za ununuzi na uhifadhi.
NB: Vigezo na Masharti kuzingatiwa.